RAIS Paul Kagame wa Rwanda amechaguliwa na chama chake cha Rwandan Patriotic Front
(RPF) kuwa mgombea urais katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Julai 7, 2024.
Kagame amekuwa rais tangu mwaka 2000, jana Jumamosi alichaguliwa kwa asilimia 99.1 ya kura kulingana na taarifa ya chama hicho.
Akihutubia chama hicho baada ya kuidhinishwa kuwa mgombea, kagame aliwashukuru wanachama kwa kuendelea kumuamini.
“Tunajua nchi hii imetoka wapi, nashukuru kwa nafasi ambayo mmecheza katika hilo.
Pia ninashukuru imani yenu ambayo kila mara na mnaendelea kuniwekea,” Kagame alisema baada ya kupitishwa,”
“Mzigo mlionipa niubebe nimekubali kuubeba. Lakini nataka wa kunitua mzigo nilioubeba na watakaoubeba wapo miongoni mwenu,” Kagame aliwaambia wanachama wenzake.