Kagera wafikia sensa asilimia 97

WAKATI leo ndiyo tarehe ya mwisho ya Sensa ya Watu na Makazi nchini, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila, amesema mkoani kwake wamefanikiwa kwa asilimia 97.4.

Alisema makadirio yaliyokuwa yamefanywa na mtakwimu mkuu wa serikali, ni kufikia kaya 644,655 za mkoa wa Kagera, ambapo mpaka leo Agosti 29, 2022 saa mbili asubuhi kaya 631,858 zilikuwa zimefikiwa na kwamba kaya zilizosalia zitafikiwa leo.

Alitaja baadhi ya changamoto  ni kukosekana umeme kwa baadhi ya vijiji, hivyo taarifa zilichelewa kutokana na vishikwambi kuzimika, lakini walifanikiwa kukodi jenereta pamoja na kununua power bank, ili kurahisisha utendaji kazi.

Pia alisema changamoto nyingine ni visiwani Wilaya ya Muleba, ambako kuna visiwa vingi hivyo miundombinu ilisumbua kiasi, lakini walifanikiwa kuitatua.

Amesisitiza kuwa hakuna mwananchi atakayesahaulika na kila mtu atahesabiwa, na kusisitiza wale wachache ambao hawajafikiwa anaamini watahesabiwa leo.

Habari Zifananazo

Back to top button