Kagera yaachana na Makame

KLABU ya Kagera Sugar imethibitisha kuacha na aliyekuwa kiungo wao Abdulaziz Makame baada ya makubaliano ya pande zote.

Taarifa iliyotolewa leo na klabu hiyo kupitia idara ya mawasiliano imeeleza kuwa Makame alisaini mkataba wa miaka miwili Julai, 2022, hivyo kuanzia leo sio mchezaji wao tena.

“Klabu inamshukuru Makame kwa huduma yake aliyotoa kwa kipindi chote cha msimu mmoja, alichokuwa akiitumikia klabu hii, tunamtakia kila la heri katika maisha yake ya soka aendako”. Imeeleza taarifa hiyo.

Makame aliwahi kuzitumikia klabu za Mafunzo ya Zanzibar, Young Africans, Namungo, Kagera Sugar.

Habari Zifananazo

Back to top button