Kajala: Roho mbaya haijengi

DAR ES SALAAM: Msanii wa filamu nchini Frida Masanja ‘Kajala’  ameiasa jamii kuacha roho mbaya na chuki binafsi pale mtu anapopata jambo zuri katika maisha yake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Kajala ameandika kuwa unatakiwa kuacha chuki, husda na roho mbaya hazina mpango katika maisha, muda wako utafika.

“Roho ya Mwanadamu inabeba mengi  lakini cha kumuomba Mwenyezi Mungu ni kuomba roho yako isibebe husda, chuki, tamaa, roho mbaya na usiwe na roho ya kupaparika yani ukiona jambo zuri kwa mwenzio unakuwa huna amani linakuvuruga,”amesema Kajala na kuongeza

“Kabisa unajiuliza kwanini yeye kwanini asiharibike, kwanini isiwe mimi yani ukijiona na roho ya namna hiyo ujue wewe ni mchawi kasoro vifaa tu vya kutendea kazi,”amesema Kajala na kuongeza

“Roho za namna hiyo zinahitaji maombi  na dua nyingi sana, tujizuie,”amesema

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button