VIJANA waliochaguliwa kujiunga na Shule ya Polisi Moshi (MPA) wametakiwa kudumisha nidhamu kwa kiwango cha juu katika sehemu zao za kazi. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Wilbrod Mutafungwa ameeleza.
Kamanda Mutafungwa ameyasema hayo leo 28, Machi 2023 katika jengo la ofisi yake Wilaya ya Nyamagana wakati akiwaaga vijana hao wanaoenda shule ya polisi Moshi kwaajili ya Mafunzo.
Mutafungwa amewataka vijana hao amewasihi kwenda kuzingatia mafunzo ya kazi watakayoyapata ili watakapohitimu waweze kutoa huduma bora kwa jamii kwa mujibu wa miongozo, taratibu na sheria.
Aidha amewasifu vijana hao kwa kutanguliza uzalendo na kuwasisitiza kuitumikia nchi yao kwa moyo wote wawapo sehemu zao za kazi mara baada ya kuhitimu.
Comments are closed.