Kamati ya Amani yampongeza Rais Samia uendelezaji miradi

MWENYEKITI wa Kamati ya Amani Tanzania, Azim Dewji amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumalizia miradi iliyoanzishwa na mtangulizi wake, John Magufuli.

Azim ambaye ni mfanyabiashara maarufu, aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Saalam jana kuwa Rais Samia amefanya kazi nzuri kumaliza utekelezaji wa miradi mikubwa iliyoanzishwa na Magufuli huku pia akianza miradi yake.

“Unaweza kuona kama ni jambo rahisi lakini ukweli si jambo rahisi hata kidogo. Mama Samia anastahili pongezi kwa kumalizia miradi mikubwa ya mtangulizi wake na kisha yeye kuanza na ya kwake,” alisema Dewji.

Alitoa mfano wa mradi wa ujenzi wa Ikulu ya Chamwino ambao uliasisiwa na Magufuli na utekelezaji wake kumaliziwa na Rais Samia. Pia alisifu usikivu wa Rais Samia katika kutatua mgogoro wa wafanyabiashara wa Kariakoo na kusema kwa utekelezaji wa pamoja alimuagiza Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa ambaye alitatua mgogoro huo.

Katika hatua nyingine, Azim aliwasihi wanasiasa wa upinzani kuwa makini na kauli zao kwa maslahi mapana ya taifa. “Wanasiasa wa upinzani wamekuwa wakijisahau na kutoa kauli za kichochezi wakiwa kwenye majukwaa yao,” alisema na kutoa mfano wa mgogoro wa Ngorongoro ambao kulikuwa na ushawishi wa wakazi kwenye hifadhi hiyo kugoma kuhama.

Alisema lakini sasa wananchi ndio wanataka kuhama kitu ambacho wapinzani hawana uwezo wa kuwahamisha.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x