Kamati ya bunge yasifu uwekezaji gesi Mtwara

KAMATI Ya Kudumu ya Bunge Hesabu za Serikali (PAC) imesema uwekezaji ambao umefanywa na serikali katika shughuli za uzalishaji wa gesi asilia na uendeshwaji wa mitambo ya kuchakata gesi hiyo katika miradi ya gesi iliyopo mkoani Mtwara umeonyesha thamani ya pesa.

Kamati hiyo imeeleza hayo leo mara baada ya kutembelea katika visima vya gesi asili vya Mnazi Bay na Kiwanda cha Kuchakata Gesi Asilia cha Madimba Mkoani Mtwara.

Advertisement

“Sisi kama kamati ya Bunge ya Hesabu za serikali tumeona value for money katika uwekezaji huu mkubwa wa miradi ya gesi ambao serikali imefanya,” amesema mjumbe wa Kamati hiyo Bonaventura Kiswaga.

Kiswaga amesema kamati hiyo itaishauri serikali kuongeza bajeti Kwa ajili ya kuendeleza miradi hiyo ya gesi asilia.

“Tunaipongeza Serikali Kwa uwekezaji huu mkubwa na wenye tija tunaiomba iendelee kuwekeza kwenye mitambo ili kuhakikisha kwamba wanachakata gesi nyingi na kuuzia pia nchi za jirani,” amesema.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Japhet Hasunga amesema kamati imeridhishwa na uwekezaji kwenye Miradi ya gesi na kusema kuwa fedha nyingi ambayo iliidhinishwa kwenye bajeti imetumika katika kusafirisha gesi kwenda Dar es Salaam Kwa ajili ya kuzalisha umeme.

Katika hatua nyingine, Hasunga amesema kamati hiyo imetembelea miradi ya gesi hiyo kuangalia kama fedha iliyoidhibishwa na Bunge kwenye miradi hiyo zilivyotumika na manufaa yake na endapo zimeleta tija katika matumizi fedha za umma.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *