KAMATI ya Utekekezaji Jumuiya ya Wazazi  CCM Dar yanolewa

VIONGOZI wa Kamati ya utekekezaji Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Dar es Salaam wametakiwa kufanya kazi itakayoacha alama, kwa  kuzingatia kanuni, ilani ya Chama na miongozo ya Jumuiya.

Hayo yamesemwa leo Januari 12, 2022 na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam,  Khadija Ally katika mafunzo ya siku tatu ya viongozi 11 wa Kamati ya utekekezaji, yaliyoanza leo katika hotel ya Star Breeze Kigamboni, jijini Dar Es Salaam.
Khadija amesema, licha ya kuchaguliwa kuongoza Jumuiya hiyo ni muhimu kupata mafunzo ya uongozi ili kila mmoja ajue mipaka yake.
“Wengi Wetu tunaingia kwenye uongozi kutokana na ushabiki au mapenzi na kitu lakini hatujui mipaka yetu ya uongozi, haiba ya uongozi, hivyo mafunzo haya yatatujengea uelewa wa pamoja.” Amesema
Amesema, mafunzo hayo ni endelevu ambapo yameanzia katika ngazi mkoani yatashuka wilyani mpaka kwenye Kata.
Nae,  Katibu wa Siasa Organization Wazazi CCM Taifa, Said King’eng’ena akiwanoa viongozi hao, aliwataka kuheshimu miiko ya uongozi na kuacha ‘showoff ‘.
” Kuna watu wameomba nafasi kwa show off, Mimi mjumbe wa Baraza, Mimi Mnec, then? ” Alihoji na kuongeza
“Mnawajibu wa kufanya kazi kwa kuzingatia sherua na kanuni, nafasi yako haina tija msipofanya kazi mnazopaswa kufanya, kuheshimu miongozo, kanuni na nidhamu, vikikosekana hivyo ni
 hatari. “Amesisitiza
Kwa upande wa Mjumbe wa Halmashauri CCM Taifa, Juma Simba Gadafi amesema mafunzo hayo yawe chachu ya kuufanya Mkoa wa Dar es Salaam unakua ngome ya CCM.
Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *