Kampuni 28 kuwekwa huru wiki hii – Mchechu

ARUSHA: Jumla ya kampuni 28 za serikali likiwemo Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) yatakuwa huru wiki hii, afisa mwandamizi wa serikali amesema Jumamosi jijini Arusha.

Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu alimwambia Rais Samia Suluhu Hassan katika kikao kazi kilichowakutanisha Mwenyekiti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma mkoani Arusha kuwa makampuni hayo sasa yatakuwa huru na kuachana na utegemezi kutoka Serikali Kuu.

Taasisi hizo ambazo majina yake yote hayajawekwa hadharani ni pamoja na Vyuo 13 vya Elimu ya Juu vya Umma. Mchechu alisema maendeleo hayo mapya ni matokeo ya mabadiliko yanayoendelea katika taasisi za umma nchini kote.

“Tumefikia muafaka na Wenyeviti na Wakurugenzi wa taasisi hizi. Tunataka kuona makampuni mengi yanafanya kazi kwa uhuru,” alisema.

Mchechu aliendelea kubainisha kuwa baadhi ya taasisi hata hivyo zimeomba kuongezewa muda wa hadi miaka miwili ili kuwa huru kikamilifu.

Taarifa kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina zinaonyesha kuwa Rais anatarajiwa kutoa tuzo kwa baadhi ya makampuni yaliyofanya vizuri katika mwaka wa fedha 2022/23.

Habari Zifananazo

10 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button