Kampuni uchimbaji madini yatoa ajira 1,000 makundi maalum

WATU 1000 walioko katika makundi ya watu wenye ulemavu, akina mama ,vijana na wazee wamepata ajira isiyo rasmi katika Kampuni ya Franone Mining and Games Stone ,inayochimba Madini ya Tanzanite katika Kitalu CĀ  katika Mji Mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara.

Makundi hayo yamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwani wamepata ajira tofauti na ilivyokuwa awali na kusema kuwa uwekezaji uliofanya na Kampuni hiyo umeweza kuwainua kiuchumi.

Wakizungumza kwenye mgodi huo hivi karibuniĀ  baada ya Waziri wa Madini, Antony Mavunde kutembelea walisema kuwa baadhi ya wamiliki wa Migodi ya Tanzanite wamekuwa wakiwanyanyapaa kwa kutowapa ajira isiyo.

Hivyo mwekezaji mzawa Onesmo Mbise amekuwa akiwajali na kuwapa ajira.

Mmoja wa wafanyakazi aliyejitambulisha kwa jina la Nai Leyani ambaye ni kiongozi wa kikundi cha akina mama wa jamii ya kifugaji ya Kimasai alisema kampuni hiyo Inapaswa kulindwa serikali ikiwa ni pamoja kuwapa elimu wachimbaji wadogo ili kuondokana na tatizo la mitobozano ndani ya migodi.

Alisema pasipo serikali kuangalia kwa jicho la tatu mwekezaji hatoweza kuendelea na shughuli za uchimbaji kwa sababu wachimbaji wadogo wanadaiwa kuendelea kuchimba kuelekea kwenye kitovu cha Kitalu C.

Joram Madole mwakilishi wa wazee walionufaika na uwekezaji huo amesema awali wakati wa Mwekezaji Mzungu walikuwa hawawezi kuingia kufanyakazi lakini sasa hivi wanafanyakazi kwa amani na utulivu na wanajipatia kipato cha kuwasomeshea wajukuu zao.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Kampuni Franone Mining ,Vitus Ndakize alisema kampuni hiyo imeweza kutoa ajira rasmi 386 na ajira 1000 ambazo siyo rasmi ambao ni wachekechaji na kazi yao kubwa ni kuchekecha udongo ambao unatoka chini ya mgodi na kwa kufanya hivyo wanajipatia riziki zao ambazo zinawasaidia katika kujikimu katika maisha yao

Alisema kupitia mgodi huo wameendalea kushirikiana na jamii inayowazunguka kwa kuchangia michango mbalimbali ya maendeleo katika Mji wa Mirerani,Wilaya ya Simanjiro na Mkoa ikiwemo ukarabati wa barabara kiwango cha changalawe kutoka getini hadi mgodini hapo ili iweze kupitika Kwa urahisi.

Habari Zifananazo

Back to top button