KAMPUNI ya China Communications Construction (CCCC), imeingia makubaliano na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ya kufadhili wanafunzi mafunzo ya vitendo.
Aidha, kampuni hiyo imetoa msaada wa vitabu ili kuendeleza utamaduni wa lugha ya Kichina chuoni hapo.
Mwakilishi Mwandamizi kutoka Kampuni ya CCCC, Zhao Zhenyuan aliingia makubaliano hayo na Mkurugenzi wa Shahada za Uzamili UDSM, Profesa Donatha Tibuhwa ambaye alimwakilisha Makamu Mkuu wa UDSM, Profesa William Anangisye alisema ufadhili huo utatolewa kwa wanafunzi wanaosoma lugha ya Kichina na utamaduni katika Taasisi ya Kichina ya Confucius iliyopo chuoni hapo.
Alisema kupitia wanafunzi hao wanaosoma lugha ya Kichina watapata nafasi za mafunzo kwa vitendo na hata kazini kwa waliomaliza chuo na wale wanaoendelea na masomo na kuwa pia kampuni hiyo itafadhili shughuli zote za kitamaduni zitakazokuwa zikifanyika chuoni hapo.
Kwa upande wake Profesa Tihubwa alisema kampuni hiyo imefanya jambo la msingi kwa wanafunzi wao hasa kipindi hiki cha mageuzi ambapo chuo hicho kinatara[1]jia kuanza kufundisha mitaala mipya inayolenga mafunzo ya kupata ujuzi.
Alisema kampuni hiyo ndiyo imejenga maktaba kubwa na ya kisasa chu[1]oni hapo na kuwa kupitia maktaba hiyo wanafunzi chuoni hapo hukua kiakili na kimaarifa hivyo huimarika kwa kiwango cha kimataifa.
Comments are closed.