Kampuni ya kubashiri kulipa wateja mabilioni

DAR ES SALAAM: Kampuni ya michezo ya kubashiri hapa nchini imelazimika kulipa kiasi cha Shilingi bilioni 53.8 kwa wateja wake baada ya kupatia matokeo waliyobashiri ndani ya siku 10 pekee.

Kwa mujibu wa kampuni ya betPawa, jumla ya wateja wake 335,706 waliibuka na ushindi baada ya kubashiri kwa usahihi matokeo ya michezo iliyochezwa ndani ya siku 10 kutoka Jumamosi, Oktoba 21 hadi Oktoba 30, mwaka huu.

“Wateja tofauti walisherehekea ushindi wakati wa mafanikio ya kuweza kubashiri kwa usahihi kwenye michezo,” imesema kampuni hiyo.

Kwa mujibu wa betPawa, aliyepata ushindi mkubwa alijinyakulia kitita cha Shilingi milioni 372.9 kwa dau la 2,200/- ikiongezewa na bonasi ya ushindi ya 645 asilimia kwenye mechi 50 alizobashiri.

“Kutokana na idadi hii kubwa ya washindi ambayo haijawahi kutokea ilisababisha ucheleweshaji wa malipo katika tasnia nzima ya michezo ya kubashiri.

“Kwetu betPawa kuwa na washindi wengi kumesababisha akaunti zetu za mitandao ya simu kulazimika kuongezwa kiwango cha pesa kila mara kulingana na kiwango cha juu kinachoruhusiwa kwa siku.

Hata hivyo tunafanya kazi saa 24 ili kumalizia malipo ya washindi wachache waliosalia,” amesema.

Baada ya wateja hao kuvuna kiasi hicho, meneja wa kampuni hiyo nchini Borah Ndanyungu amenukuliwa akisema: “Hakuna mtu bora kuliko wateja wa betPawa ambao wameweza kufanikiwa kupata ushindi MKUBWA, na katika kipindi hiki cha siku 10 wameweza kushinda zaidi kuliko hapo awali.

“Tunafahamu idadi kubwa ya ushindi umesababisha ucheleweshaji katika tasnia nzima ya michezo ya kubashiri na sisi betPawa tunafurahi kuwa tayari tumeweza kulipa washindi wengi tayari mpaka sasa. Tunafanya kazi bila kuchoka ili washindi wachache waliobakia mwisho walipwe.

Habari Zifananazo

Back to top button