Kampuni ya Ruby yaweka mkazo ajira kwa Watanzania

MOROGORO; VIJANA zaidi ya 525 wa Kitanzania wamejipatia nafasi za kazi, ambao kati ya hao 125 ni ajira za kudumu na wengine 400 wafanyakazi wa muda katika kampuni ya uchimbaji, uuzaji na ununuzi wa madini ya vito ya Ruby International Limited.

Kampuni hiyo imetoa takwimu hizo, leo kuelekea kuadhimisha miaka 10 ya kuanzishwa kwake yatakayofanyika baadaye  mwaka huu.

Kampuni hiyo yenye makao makuu yake Ulanga mkoani Morogoro, ambayo pia inahudumu Bangkok nchini Tailand ilianzishwa mwaka 2014, ambapo mpaka sasa ni miaka 10.

Akizungumza na HabariLEO, Ofisa Habari na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Elia Ngachucha amesema kwa wafanyakazi wasio na ajira ya kudumu wamepanga kuwaandalia kazi ambazo zitafanyika kwa muda mrefu angalau wapate mikataba ya muda mrefu.

“Pili baadhi ya kazi zetu sio za kudumu ndio maana na wafanyakazi wengine tunawaajiri kulingana na asili ya kazi zetu,” amesema

Amesema kampuni kwa ujumla inawahudumia wote sawa kwa kuwapa maradhi, chakula na matibabu yote na wanapotaka kujiongeza kitaaluma pia wanasaidiwa.

Habari Zifananazo

Back to top button