Kampuni ya The Guardian hatiani

ARUSHA: Kampuni ya First World Investment Court Broker ya jijini Arusha imeagizwa kukamata mali za Kampuni ya The Guardian ya Jijini Dar es Salaam baada ya kampuni hiyo kushindwa kumlipa Mfanyabiashara maarufu wa Madini ya Tanzanite jijini Arusha ,Justin Nyari kiasi cha Sh milioni 410 ndani ya siku 14.

Uamuzi huo umetolewa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Mariamu Mchomba Mei 6 mwaka huu baada ya Kampuni ya The Guardian kushindwa kesi katika Mahakama ya Rufaa chini ya majaji watatu na alitoa amri kwa Dalali Allan Mollel kupitia Kampuni yake ya First World Investment kuhakikisha anatekeleza amri ya Mahakama ya Rufaa ya kukamata mali za Kampuni ya The Guardin Kama mshitakiwa wa kwanza na mshitakiwa wa pili Kiwanda Cha uchapishaji cha Kampuni ya Printa Afrique .

Baada ya agizo hilo la Naibu Msajili Mkurugenzi wa First World Investment,Allan Mollel Mei 16 mwaka huu alimwandikia barua Naibu Msajili utekelezaji wa awali wa oda ya Mahakama ya Rufaa ya kuupa taarifa ya kusudio la kuuza mali za Kampuni ya The Guardian uongozi wa Kampuni hiyo kutakiwa kumlipa Nyari kiasi hicho cha fedha ndani ya siku hizo lakini ulishindwa kufanya hivyo hadi siku ya mwisho ya Mei 27 mwaka huu kutakiwa kulipa.

Advertisement

‘’Tafadhali rejea amri{Order} ulioitoa Mei 6 mwaka huu,Utekelezaji wake nikaufanya Mei 13 mwaka huu kwa kufika kwenye eneo husika ‘’Bulding on Plot no 122 Mikocheni service Trade Area Dar es Salaam in c.t.no 47632 in the name of Guardian limited ‘’

‘’Taratibu za uthamini zinaendelea nitawasilisha taarifa zitakapokuwa tayari na siku 14 za taarifa zitaisha Mei 27 mwa huu’’ naomba kuwasilisha taarifa ya awali ya utekelezaji kwa hatua zako muhimu’’ ilisema sehemu ya barua ya Mollel

Akizungumza na HabariLeo Dalali Mollel alikiri kutekeleza maagizo ya Mahakama ya Rufaa juu ya kampuni ya The Guardian kutakiwa kumlipa Nyari Sh milioni 410 ndani ya muda huo lakini hawakufanya hivyo hadi muda kumalizika hivyo hatua zingine zinafuata ikiwa ni kukamata mali za kampuni hiyo ya magazeti.

Akizungumza na gazeti hili, Nyari alisema anaishukuru Mahakama kwa kutenda haki.