Kampuni yajinadi uchakataji mafuta
MWEKEZAJI na mfanyabiashara wa kampuni ya kuchakata mafuta ya Wild Flower and Grans Oil , Azizi Ally amesema wanatarajia kufikia kiwango kikubwa cha uzalishaji mafuta tani 560,500 kabla ya malengo ya serikali ya 2027.
Akizungumza na mwandishi wa Habari Leo, Azizi alisema akiwa mwekezaji mzawa, amejipanga Kutatua changamoto hiyo kwa kuhakikisha wananunua kwa wingi mali ghafi kutoka katika shambani ya wakulima na kuzichakata ili kupata mafuta ya kupikia.
Alisema wamejipanga katika kufanya uzalishaji huo mkubwa katika mkoa wa Singida kupitia zao la alizeti, ambao wanatarajia kuzalisha takribani tani 75 kwa siku.
Alisema katika kuhakikisha wanatimiza malengo ya Serikali kabla ya mwaka 2027, wanatarajia kutanua zaidi viwanda vyao katika mikoa mingine ikiwemo mkoa wa Dodoma, Shinyanga na Iringa na mikoa ya jilani.“Kiwanda cha Singida kimekamilika kwa asilimia mia moja, hivyo kinachoendelea kwa sasa nibado uzalishaji.
Tunawashukuru Kituo cha Uwekezaji na wizara husika kwa msaada mkubwa waliotupa” alisema.Alisema kituo cha Singida kikikamlika wanatarajia kutoa zaidi ya ajira 190 za moja kwa moja, lakini pia wanatarajia kuzalisha ajira ambazo sio za moja kwa moja.Alimalizia kwa kusema lengo kubwa ni kufanya uzalishaji mubwa abao utasaidia kuuza mafuta ndani nan je ya nchi.