Kampuni yatoa vifaa kukuza michezo shuleni

KAMPUNI ya Isamilo Supplies Ltd imeungana na Halmashauri ya Mji wa Geita kusaidia kuinua sekta ya michezo kwa kujitolea vifaa vya michezo kwa ajili ya shule, timu ya Geita Gold God na Geita Gold Queens.

Akizungumuza baada ya kukabidhi msaada huo, meneja mkuu wa kampuni hiyo, Robison Mageta amesema katika mpango huo shule saba za msingi pamoja na shule saba za sekondari zitanufaika.

Mageta amesema wameanza kwa kutoa vifaa vya michezo vyenye thamani ya Sh milioni 6 huku dhamira kuu ni kufikia adhima ya kuinua michezo mkoani Geita na kuziunga mkono timu zilizopo kwa sasa.

Advertisement

“Michezo ni afya, michezo ni ajira, lakini pia michezo inaleta amani lakini tutazidi kutoa kwa kadri ambavyo tutazidi kupata mahitaji, vifaa hivi tumeweka vifaa vya mpira wa miguu, pete na kikapu.”

Ameongeza kuwa, pia wametoa vifaa vya sekta ya afya ambavyo ni mashuka seti 50, pamoja na kitanda kimoja cha mama na mtoto ili kusaidia kukabiliana na vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.

Ofisa Michezo Halmashauri ya Mji wa Geita, Juliana Kimaro amesema vifaa vya michezo vitasaidia kuiunua sekta ya michezo ndani ya halmashauri na kupunguza upungufu uliokuwepo kwenye baadhi ya shule.

Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Mji wa Geita, Dk Sande Mwakyusa amewashukuru kampuni ya Isamilo kwa msaada huo kwani umesaidia kuimarisha huduma za afya ndani ya halmashauri hiyo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya MkAMji wa Geita, Zahra Michuzi amewapongeza kampuni ya Isamilo Supplies Ltd kwa kuguswa na sekta ya afya na michezo huku akiwaomba wadau wengine kuunga mkono.

“Kwenye mashule tumetoa maelekezo kwa walimu wa michezo kuhakikisha katika kila wiki moja kila mwezi vijana washiriki katika mazoezi na michezo ya kuonyesha vipaji mbalimbali.”

Amesema pia halmashauri imeweka mkakati maalum wa kufanya maboresho ya viwanja vya umma ili kutengeneza mazingira rafiki kwa wananchi waweze kuhamasika kufanya mazoezi ya viungo.

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *