Kampuni yaunga mkono utalii hifadhi ya Burigi

IMEELEZWA vinywaji vitokanavyo na mimea ya matunda katika Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera vinatarajiwa kupelekwa katika Hifadhi ya Taifa ya Burigi Chato kwa lengo kuunga mkono utalii pamoja na kukuza mshikamano baina ya jamii wawekezaji mkoani Kagera.

Akizindua kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Hlucky inayojihusisha na utengenezaji wa vinjwaji hivyo, Hamis Jumanne amesema kampuni yake imekuwa ikishirikiana na jamii kwa kuandaa mnyororo wa kukuza uchumi katika Wilaya ya Karagwe ambapo wananchi 70 hufanya kazi za vibarua kwa siku katika kiwanda chake, pamoja na waajiliwa 12 wa kudumu hivyo Ni wakati wa kudumisha ushirikiano.

Katika uzinduzi huo aliandaa michezo mbalimbali kama riadha, mpira wa miguu, mpira wa wavu na kuwahakikishia wanachi kuwa kupitia ziara hiyo ya utalii zaidi ya watu 200 watakaa hifadhini na kuona maajabu yanayopatika katika hifadhi hiyo.

Amesema kutakuwa na matukio mbalimbali ikiwemo kupiga picha ,kuona wanyama huku utalii huo ukinogeshwa na mabondia mbalimbali akiwemo Karim Mandogo ambao wataanza kuweka kambi Karagwe Septemba mwaka huu.

“Tunapata ushirikiano mkubwa kwa jamii ,wanatuunga mkono ,tunatengeneza mnyororo wa thamani katika kuhakikisha jamii inaongeza kipato,tushafanya mabonanza ya michezo minane tumekuwa tukichangia naendelea kwa nyanja mbalimbali ,lakini mimi na uongozi tumeamua kuja na kitu tofauti kwanza kuiamusha Royal Tour kama imelala huku Mkoa wa Kagera, Pili kufanya utalii kupitia mchezo wa ngumi, tatu watu kubadili mazingira na kwenda kuona wanyama.”alisema Hamis.

Alisema kuwa safari hiyo itafanyika kuanzia septemba 20 mwaka na mara baada ya burudani za hifadhini kumalizika tayari kampuni hiyo itaandaa mkanda wa ngumi wa dunia utakaowakutanisha wapiganaji maarufu katika jiji la Mwanza.

Habari Zifananazo

5 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button