Kampuni yaweka mikakati uwekezaji

Kampuni ya uwekezaji wa pamoja UTT AMIS imesema inaendelea kuboresha huduma zake ili kuwafikia wateja wengi zaidi na kuwa daraja kwa wote wenye ndoto za kuwekeza.

Kauli hiyo imetolewa leo Julai 31, 2023 kwenye mkutano wa taasisi hiyo na Jukwa la wahariri wa vyombo vya habari ikiwa ni tekelezo la agizo la Msajili wa Hazina Nehemiah Mchechu ambaye alizitaka taasisi na mashirika ya serikali kuwa na mikutano ya mara kwa mara na jukwaa hilo.

Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Simon Migangala amesema mfuko huo unawaunganisha wawekezaji wadogo na wakubwa huku wawekezaji wadogo wakipata fursa ya kunufaika sawia na wawekezaji wakubwa.

“Wewe ukiweka hata kama ni kidogo unapata sawa na kile ambacho anapata yule aliyewekeza fedha nyingi lengo letu ni kuwapa fursa ya kupata faida, tumejitahidi sana kuwafikia wananchi wadogo wadogo kwa kiasi kikubwa na hata wananchi wanahamasika”

Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa Taasisi hiyo imekuwa ikiongeza ukuaji wake kwani kwa kipindi cha miaka mitatu ukuaji wake umekua kwa zaidi ya asilimia 50 kitu ambacho kinaonyesha wazi ongezeko la watanzania juu ya dhana nzima ya uwekezaji na lengo lao ni kuendelea kufikisha huduma zao maneno mbalimbali huku pia wakienda samabamba na mabadiliko ya teknolojia jambo ambalo limesababisha urahisi zaidi wa upatikanaji wa huduma zao.

Kwa upande wake Mjumbe wa kamati tendaji wa jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) Anjella Akilimali amesema mkutano huo na kampuni hiyo umewafanya kuyafahamu mengi hivyo watakuwa daraja la kuwafikishia wananchi elimu juu ya uwekezaji huo.

Mbali na kukua huko bado kampuni hiyo inakabilkiwa na changamoto ya baadhi ya watu kukosa elimu ya umuhimu wa kuwekeza UTT hivyo imedhamiria kushirikiana kwa dhati na vyombo vya habari ili kufikisha elimu kwa jamii.

Habari Zifananazo

8 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button