Kampuni zanufaika mradi ujenzi wa zahanati

BAADHI ya kampuni za ujenzi za wazawa zimenufaika na miradi inayotekelezwa na mgodi wa Barrick Bulyanhulu ukiwemo mradi wa ujenzi wa zahanati unaojengwa katika kijiji cha Bushing’we kata ya Bulyanhulu Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga.

Zahanati hiyo imejengwa kwa Sh milioni 88 fedha ambazo ni msaada kutoka kwenye mgodi huo bila wananchi kuchangia chochote.

Advertisement

Akiongea na waandishi wa habari leo Juni 16, 2023 mratibu wa kampuni ya ujenzi ya mjasilia, Thomas Mshiru amesema wapo katika ukamilishaji wa zahanati hiyo baada ya kupata.

“Tumefaidika mambo mengi,tumejifunza mitambo na uwepo wa Mgodi umesaidia wao kupata kazi nakutoa ajira za muda mfupi kwa watu zaidi ya 100.” amesema Bashiru.

Msimamizi wa Kampuni hiyo, James Masatu amesema wamepata kazi kupitia kampuni hii amefaidika kuboresha maisha na kuipongeza kampuni ya Barrick Bulyanhulu kwa kuweza kutambua umuhimu wa kutumia wakandarasi Wazawa.

Mrakibu Idara ya Mahusiano kutoka kwenye mgodi huo, William Chungu ameeleza wameamua kutoa fedha hizo kujenga zahanati ambazo hazihusiani na fungu la fedha za huduma kwa jamii (CSR).

Meneja wa umoja wa vijiji 14 vinavyozunguka mgodi huo, Joseph Lubega amesema wamewafikia kuwatafutia ajira watu zaidi ya 1000 wanaotoka kwenye maeneo yanayozunguka mgodi huu.

“Kampuni za kizawa zinazo pata zabuni za ujenzi kupitia Mgodi wa Barrick Bulyanhulu zinapewa watu wakufanya kazi za muda mfupi ili waweze kujipatia kipato”amesema Lubega.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *