Kampuni150 kushiriki maonesho ya ubunifu Dar es Salaam
ZAIDI ya kampuni 150 za wabunifu zitashiriki katika maonesho ya ubunifu yatakayofanyika tarehe 13 na 14 Oktoba mwaka huu katika Makubusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Sahara Venture,Musa Kamata aliyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Amesema maonesho hayo yenye jina la Sahara Spacks ni tukio linalojihusisha na masuala ya ubunifu, ujasiliamali,uwekezaji na teknolojia ambapo tangu mwaka 2016 wamekuwa wakiandaa tamasha hilo.
“Na mwaka huu tumejipanga vizuri na tuna mikakati tofauti lengo kubwa tunataka kuonesha nini vijana wa kitanzania wanataka kufanya,tutakuwa na maonesho ambayo yataanza ijumaa ya wiki hii na jumamosi Makumbusho ya Taifa lakini tunashukuru kwa sapoti kutoa serikali na kutoka tume ya taifa ya sayansi na teknolojia wamekuwa chachu kubwa kwenye masuala ya ubunifu,”ameeleza,
Amebainisha kuwa lengo la maonesho hayo ni kuhakikisha wanawashirikisha wadau mbalimbali kwani kuna mabadiliko mengi na teknolojia inakua na vitu vimebadilika hivyo wanahakikisha watanzania wanaenda nayo.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknoloji (COSTECH) Samson Mwela amesema wamekuwa mstari wa mbele katika kukuza ubunifu ambapo hadi sasa wamesaidia wabunifu 83 na baadhi yao watakwenda katika hilo tukio.
“Tunaendeleza bunifu za ndani zile bidhaa ziweze kuwafikia wananchi na kuleta mabadiliko hili tukio COSTECH imekuwa ikishiriki kama mdau muhimu na kutakuwa na mada kadhaa ambazo zitajadiliwa.
Naye Meneja wa Sahara Spacks,Rose Urassa amesema wanafanya maonesho kila mwaka kwaajili ya kuweka na kuwaunganisha wadau mbalimbali katika kuwekeza mabadiliko yanayokuja na teknolojia.