Kane United? Spurs hawataki

UHAMISHO wa Harry Kane kwenda Man United huenda usifanikiwe baada ya Tottenham Spurs kuamua kutomuuza mshambuliaji huyo raia wa England. Mtandao wa Sky Sport umeripoti.

Mkataba wa Kane umebaki mwaka mmoja Spurs, hivyo kama msimu ujao ataendelea kubaki tafsiri yake atakuwa mchezaji huru, na kuanzia hapo atakuwa huru kuamua sehemu ya kwenda bila ada yoyote.

Ukiwa kama mbadala wa Kane, United imeripotiwa inataka kumsajili mshambuliaji wa Napoli, Victor Osimhen ambaye ndiye straika anayetajwa sana katika soko la usajili kwa sasa.

Advertisement

Kwa mujibu wa Sky Sport, United ina mpango wa kuleta washambuliaji wawili, mmoja mwenye uzoefu na mwingine kwa ajili ya misimu ijayo na tayari wameanza mazungumzo na nyota wa Atalanta, Rasmus Hojlund mwenye miaka 20.