Kanisa laendesha maombi kwa Taifa

Kanisa laendesha maombi kwa Taifa

WAUMINI wa Kanisa la Calvary Assemblies of God la jijini Dar es Salaam, wameendesha maombi maalum ya amani kwa ajili ya Taifa na viongozi wake.

Maombi hayo yalifanyika jana na kuendeshwa na Mchungaji  kiongozi wa kanisa hilo, Imelda Maboya katika ibada maalum ya kuliombea taifa na viongozi iliyofanyika kanisani hapo,viwanja vya UFI Ubungo.

Pamoja na maombi hayo ya kuwatakia kila la heri viongozi wakuu wa nchi, waumini hao kupitia kwa Mchungaji Kiongozi, Imelda Maboya waliiomba serikali kuwasaidia waendelee kubaki katika eneo lao.

Advertisement

Mchungaji huyo alisema japokuwa wako katika eneo hilo kwa zaidi ya miaka 22, wameanza kutatizwa na wavamizi wanaowataka waondoke haopo.

“Mahali hapa lilipo kanisa kulikuwa ni kichaka cha wavuta bangi, walevi na wahuni wengine, kanisa limesaidia kuiondosha hali hiyo,” alisema na kuongeza kuwa wakati wanapewa walielezwa kama ikitokea patauzwa watapewa kipaumbele.