Kanisa laporomoka na kuua tisa wakati wa Ibada

MEXICO: Takriban watu tisa – wakiwemo watoto watatu – wameuawa na makumi wengine wakibaki wamenasa kwenye vifusi baada ya paa la kanisa kuanguka wakati wa misa ya Jumapili kaskazini mwa Mexico.

Maafisa wamesema watu 40 walijeruhiwa na kupelekwa hospitali kwa matibabu – ikiwa ni pamoja na mtoto wa miezi minne, watoto watatu wa miaka mitano na wawili wa miaka tisa – huku waumini wengine 30 wakiwa hawajulikani waliko.

Ofisi ya msemaji wa usalama wa serikali ilisema kuwa kuporomoka kwa paa hilo kunawezekana kulisababishwa na “tatizo la jengo”.

Advertisement

Vitengo vya walinzi wa kitaifa, polisi wa serikali, ofisi ya ulinzi wa raia na Msalaba Mwekundu wako kwenye eneo la tukio.

Waokoaji wamekuwa wakifanya kazi usiku kucha kutafuta manusura wanaoaminika kuwa chini ya vifusi.

Askofu Jose Armando Alvarez alisema paa liliporomoka wakati waumini wa kanisa la Santa Cruz katika mji wa pwani wa Ghuba wa Ciudad Madero, karibu na mji wa bandari wa Tampico.

Pia alitoa wito kwa yeyote ambaye alikuwa na mbao kuchangia ili kuinua tena paa hilo huku vikosi vya uokoaji vikinyakua magofu.

Mbwa waliofunzwa maalum pia wametumwa kwenye vifusi kutafuta manusura.

1 comments

Comments are closed.

/* */