Kanisa: Tusaidie wenye uhitaji maeneo tunayoishi

ARUSHA; KANISA la Tanzania Assemblies of God (TAG), GalileeTemple lililopo Ngaramtoni Arusha limeadhimisha miaka 85 ya kuanzishwa kwake na kutoa msaada wa vyakula kituo cha watoto kiitwacho Mama Safi.

Akizungumzia kuhusu maadhimisho hiyo, Prof. Solomon Mwagisa ambaye ni Askofu wa Kanisa hilo, ameishukuru serikali kwa ushirikiano wanaotoa katika masuala ya dini na kusisitiza jamii kurudisha fadhila kwa jamii zenye uhitaji katika maeneo mbalimbimbali wanayoishi.

Pia amekemea vitendo vya ukatili kwa wanawake, watoto na jamii kwa ujumla ikiwemo kudumisha upendo kwa rika mbambali, kwani jamii yenye upendo huleta umoja na amani

“Siku ya leo ni njema na ina ujumbe wa kukumbuka tulipotoka kufikia miaka 85 ya kanisa si jambo dogo, tunamshukuru Mungu lakini kubwa zaidi tukumbuke watu wenye mahitaji maalumu, ikiwemo kuiombea serikali na viongozi, wake zaidi tudumishe amani,” amesema.

Naye Mchungaji Msaidizi wa kanisa hilo, Daniel Solomon amesema kanisa linaendelea kushirikiana na serikali katika mambo mbalimbali hususan jamii kwa kutoa elimu ikiwemo utoaji huduma kwa watu wanaoishi mazingira duni, wajane na wenye mahitaji muhimu.

 

Habari Zifananazo

Back to top button