Kapinga awapa maagizo TGDC

NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameitaka kampuni ya Uendelezaji wa Joto Ardhi Tanzania (TGDC) kuzalisha umeme kwa kutumia rasilimali ya jotoardhi ili kuunga mkono mpango wa Serikali wa kuwa na nishati safi na endelevu.

Waziri Judith ametoa agizo hilo wakati wa kikao cha Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni hiyo pamoja na menejimenti ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa ziara yake ya kikazi ya kukutana na baadhi ya taasisi na kampuni zilizo chini ya wizara ya nishati kwa lengo la kuona utendaji kazi wa taasisi hizo.

“Kama ambavyo Serikali imejipambanua kuwa inatekeleza mpango wa nishati safi na endelevu, ni wakati wa TGDC sasa kuonesha uwezo na ubunifu wenu katika kufanikisha hilo ili kutoa mchango mkubwa kwa taifa.

” alisema naibu Waziri.

Aidha amesema, kufanikisha kwa mpango huo wa kuzalisha umeme kwa kutumia rasilimali ya jotoardhi itaondoa changamoto ya umeme unayoikumba nchi kwa kuzingatia kuwa nishati ya Jotoardhi ni endelevu.

Habari Zifananazo

Back to top button