Kapombe amfagilia Rais Samia

Simba kusukwa upya

BEKI wa Simba, Shomari Kapombe amesema mfumo alioanzisha Rais Samia Suluhu Hassan kununua bao kwa timu za Simba na Yanga kwenye michuano ya kimataifa una maana kubwa katika soka la Tanzania.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuelekea mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya leo, Kapombe alisema mfumo huo wa kutoa fedha kwenye mechi kubwa unasaidia kutoa motisha kwa wachezaji na kwamba utasaidia kuzikuza timu na mpira wa nchi.

“Kama wachezaji wa Simba tunamshukuru Rais Samia kwa sapoti kubwa anayoonesha kwa hizi timu zetu, sisi tumeipokea vizuri na niseme kuna kitu anakileta na kitasaidia kukuza mpira wa Tanzania,” alisema Kapombe na kuongeza:

Advertisement

“Akiendelea na hamasa za namna hii katika mashindano makubwa hakika tutakuwa juu katika mpira wa Tanzania.”

Tangu atangaze kununua kila bao litakalofungwa na Simba na Yanga katika michuano ya kimataifa tayari wachezaji wa klabu hizo washanufaika.

Yanga imevuna Sh milioni 30 baada ya kufunga mabao sita, katika michezo mitatu dhidi ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) walishinda mabao 3-1 na dhidi ya Real Bamako ya Mali walishinda jumla ya mabao 3-1 katika michezo miwili ya nyumbani na ugenini.

Simba ilivuna Sh milioni 10 baada ya kufunga mabao mawili katika michezo miwili iliyoshinda dhidi ya Vipers ya Uganda ikishinda jumla ya mabao 2-0, bao 1-0 ugenini na 1-0 nyumbani.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *