Kapombe, Tshabalala waongezwa Stars

Stars wapo kamili kuiua Uganda

WACHEZAJI Shomari Kapombe na Mohamed ‘Tshabalala’ wa Simba wamerudishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, ambacho kinajiandaa na mchezo wa marudiano wa kufuzu fainali za Afcon 2023 dhidi ya Uganda.

Akizungumza na waandishi wa Habari, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Wallace Karia amesema sababu ya kuwarejesha wachezaji hao ni kupunguza maneno ya mashabiki ambao walikuwa wakilalamika kuhusiana na wachezaji hao kutojumuishwa kwenye timu hiyo.

“Maneno yalikuwa mengi sana baada ya uteuzi uliofanyika mwanzoni, lakini tumeona matunda yake, kuongezwa kwa Kapombe na ‘Tshabalala’ ni pendekezo la Kocha Mkuu, Adel Amroache na tayari wamejiunga kambini na wenzao,” alisema Karia.

Advertisement

pharmacy

Wachezaji hao walikosekana kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichoifunga Uganda ‘The Cranes’ bao 1-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika Ijumaa iliyopita nchini Misri.