Karia aguswa kifo cha Madega

Rais wa TFF, Wallace Karia.

RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia ametuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa zamani wa Yanga Iman Madega ambaye amefariki dunia leo.

“Natuma salamu zangu za rambirambi kwa familia ndugu, jamaa na marafiki, na wote walioguswa na msiba.

” Imeeleza taarifa hiyo.

Advertisement

Taarifa ya TFF, iliyotolewa leo imeeleza kuwa mchango wa Madega utakumbukwa daima.

Madega aliwahi kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Pwani, Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji TFF, na Mwenyekiti wa Yanga.