WATANZANIA waliokuwa katika Jamhuri ya Sudan wameanza safari ya kurejea nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ethiopia, Bole ambapo Shirika la Ndege la ATCL litawasafirisha hadi katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Raia hao ni pamoja na Wanafunzi 150, watumishi wa Ubalozi 28 na wanadiaspora 22.
Waliondolewa Khartoum, Sudan kwa usafiri wa magari hadi Ethiopia ambapo wameanza safari ya kurejea nchini.