Karume: Wahitimu Muhas kaitumikieni jamii

RAIS wa zamani wa Zanzibar, Aman Abeid Karume amewataka wahitimu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS ) kwenda kuitumikia jamii kulingana na ujuzi walioupata chuoni hapo,pamoja na kuwa waaminifu katika utendaji wao.

Kiongozi huyo amesema hayo leo katika mahafali ya 17 ya chuo hicho ambapo jumla ya wahitimu 1306  wametunukiwa Stashahada na Shahada ya masomo mbalimbali kwa mwaka 2023.

Katika wahitimu hao 43 wametunukiwa Digrii ya Uzamili wa Sayansi Maalum, 197 Digrii ya Uzamili ya Udaktari wa Binadamu, 12 wametunukiwa Digrii ya Uzamili ya Sayansi ( Skuli ya Tiba ).

Wahitimu 14 wametunukiwa Digrii ya Uzamili ya Udaktari wa Kinywa na Meno, 11 Digrii ya Uzamili na Ufamasia, 4 Digrii ya Uzamili ya Udhibiti na Uangalizi wa Usalama wa Madawa na Famakoepidemiolojia. Wahitimu 108 wametunukiwa Digrii ya Uzamili ya Sayansi ya Afya ya Jamii.

Wahitimu 7 wametunukiwa Digrii ya Uzamili ya Sayansi ya Afya ya Jamii, 6 wametunukiwa Digrii ya Uzamili ya Maadili, 2 Digrii ya Uzamili ya Sera za Afya na Menejimenti, 57 Digrii ya Uzamili ya Sayansi ( Skuli ya Sayansi ya Afya ya Jamii).

Htaa hivyo wahitimu 22 wametunukiwa Digrii ya Uzamili ya Sayansi-Skuli ya Uuguzi na wawili wametunukiwa Digrii ya Uzamili ya Sayansi za Afya kwa njia ya Utafiti na Machapisho na wengineo kwenye masomo mbalimbali.

Awali akizingumza Mwenyekiti wa Baraza la Muhas, Harrison Mwakyembe alisema chuo hicho kinajiandaa kujenga Campas mpya mkoani kigoma na ujenzi unaanza mwakani, utachukua miaka miwili.

Habari Zifananazo

Back to top button