Katavi mambo mazuri sensa

MKUU wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuf amesema hadi mchana wa leo, shughuli ya sensa inaendelea vizuri katika wilaya hiyo.

Amesema hadi sasa hakuna changamoto yoyote iliyojitokeza na kuripotiwa, hivyo mambo yanaenda vizuri.

Karani wa Sensa Kata ya Ilembo yalipo makazi ya Mkuu huyo wa Wilaya, Emile Kimambo amesema zoezi hilo linahitaji ushirikiano wa karibu kutoka kwa wananchi, ili  lifanyike kwa ufanisi.

Kwa upande wake, Meya wa Manispaa ya Mpanda, Haidary Sumry, mara baada ya kuhesabiwa amesema zoezi la kuhesabu, awamu hii liko tofauti na miaka ya nyuma, kwani maswali yanayoulizwa hakika yanalenga kutatua changamoto za wananchi.

“Yapo maswali ya maji, namna wanachi tunavyopata huduma za maji, tunayapata kwenye maeneo gani, ni maswali ambayo unaona kabisa yanalenga kujua ukubwa wa tatizo au ukubwa wa mafanikio,” alisema Haidary Sumry

Habari Zifananazo

Back to top button