Katavi yafungua fursa mpya uwekezaji madini

AFISA Madini Mkazi wa Mkoa wa Katavi, Mhandisi Andrew Mwalugaja amewakaribisha wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi kuchangamkia fursa katika Sekta ya Madini, akibainisha kuwa mkoa huo umebahatika kuwa na rasilimali za madini zikiwemo dhahabu, shaba, risasi, fedha, nikeli, manganese na madini ya ujenzi.

Akizungumza katika mahojiano maalum, Mhandisi Mwalugaja amesema ofisi yake imeendelea kuongeza ushiriki katika Sekta ya Madini kupitia utoaji leseni mpya, zikiwemo leseni tatu za utafiti katika mwaka wa fedha 2025/2026 kati ya Julai na Oktoba 2025 katika Wilaya za Mpanda, Tanganyika na Mlele, leseni 19 za uchimbaji wa kati, pamoja na leseni 290 za uchimbaji mdogo.

SOMA: Wizara ya Madini waja kisasa zaidi

Ameongeza kuwa utoaji wa leseni za biashara ya madini nao umeimarika, ambapo mwaka wa fedha 2024/2025 jumla ya leseni 107 zilitolewa, 35 za biashara kubwa ya madini na 72 za biashara ndogo ya madini.

Tangu kuanza kwa mwaka wa fedha 2025/2026 mapema Julai hadi Oktoba, leseni 82 za biashara ya madini zimetolewa zinazojumuisha leseni kubwa 34 na ndogo 48.

Amesema Serikali imeanzisha masoko mawili ya madini katika Manispaa ya Mpanda na eneo la Karema ili kuhakikisha wachimbaji wanapata soko la uhakika, huku mazingira ya uwekezaji yakiendelea kuimarika kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa katika kuongeza usalama na mifumo rafiki kwa wawekezaji.

Ameeleza kuwa Sekta ya Madini imeendelea kuleta mafanikio makubwa, hususan katika ongezeko la maduhuli ya Serikali kutoka Sh bilioni 1.16 mwaka 2017/2018 hadi Sh bilioni 9.26 mwaka 2024/2025.

Katika kipindi cha Julai hadi Oktoba 2025 pekee, Sh bilioni 3.80 tayari zimekusanywa sawa na asilimia 38 ya lengo la mwaka la Sh bilioni 10.

Wadau wa madini katika mkoa huo wamepongeza juhudi za Serikali kuboresha mazingira ya uwekezaji, wakibainisha kuwa maboresho ya miundombinu, utatuzi wa changamoto kwa haraka na upatikanaji wa huduma za kiserikali kwa wakati.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Google provides awesome remote work opportunities, allowing me to earn $2000-$3000 weekly with just 2-4 hours of daily work. It’s been a game-changer, offering flexibility and reliable income. If you’re seeking a genuine way to earn online, don’t miss this chance. Start today and transform your life!
    .
    More Details For Us →→ http://www.big.income9.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button