Katibu RFEF afutwa kazi
SHIRIKISHO la soka Hispania limemfuta kazi Katibu Mkuu, Andreu Camps na kuomba radhi kwa kilichotokea baada ya fainali ya Kombe la Dunia la Wanawake.
–
“RFEF inafahamu hitaji kamili la kuanza hatua mpya na kufunga mzozo wa kitaasisi ulioanza baada ya ushindi wa timu ya taifa katika Kombe la Dunia,” shirikisho hilo lilisema.
–
Hapo awali, wachezaji wengi walikubali kusitisha kugomea timu ya taifa.
–
Wachezaji walianza kususia baada ya rais wa wakati huo wa RFEF, Luis Rubiales kumbusu mshambuliaji, Jenni Hermoso kufuatia ushindi wa Hispania dhidi ya Uingereza katika fainali ya Kombe la Dunia la Wanawake Agosti 20, 2023.
–
Pia iliomba msamaha kwa kuwaweka wachezaji katika hali zisizohitajika na haswa kwa Hermoso kwa kuingia katika mazingira ambayo hakuyategemea.
–
“Tunaelewa kwamba wachezaji wanahitaji kuhisi kuwa shirikisho ni nyumbani kwao, mazingira salama ambapo wanaweza kuonesha taaluma yao na ubora wa michezo huku wakionesha kwa upendo kuiwakilisha Hispania,” RFEF ilisema taarifa hiyo.
–
Mbali na kuondoka kwa Camps, Reuters ikinukuu chanzo cha RFEF, imeripoti kati ya viongozi sita hadi tisa wataachishwa kazi kama sehemu ya makubaliano na wachezaji.