MCHIMBAJI mdogo wa madini ya Tanzanite Anslemu Kawishe amepata Sh bilioni 2.2 baada ya kuuza vipande viwili vya Tanzanite kwenye hafla iliyo hudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Madini Dk. Dotto Biteko na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Laurence Luoga.
Mwezi Juni 2020, Mchimbaji madini Laizer Kuryani ametajwa kuwa bilionea mkubwa baada ya kupata mawe mawili ya Tanzanite. Serikali kupitia Benki kuu iliyanunua mawe hayo kwa gharama ya Sh bilioni 7.8 jiwe moja lina kilo 9.27 na lingine lina kilo 5.8.