Kaya 367,456 kupatiwa vyandarua Mtwara, Lindi
JUMLA ya kaya 367,456 katika Halmashauri sita Mikoa ya Mtwara na Lindi, zinatarajiwa kupatiwa vyandarua vyenye dawa kupitia kampeni, ambayo inatekelezwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tamisemi kwa ufadhili wa USAID-PMI.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas amesema hayo leo wakati akizundua kampeni katika Kijiji Cha Mpwapwa Wilaya ya Newala, mkoani Mtwara, kwa niaba ya Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.
Amesema jumla ya vyandarua 812,118 vyenye dawa vitagawiwa kwa halmashauri hizo sita, ambapo halmashauri za Mtwara, Masasi na Nanyumbu zitapatiwa jumla ya vyandarua 424,711, huku Lindi, Mtama, Nachingwea na Ruangwa zikipatiwa 387,407.
Kanali Abbas amewataka wananchi kuhakikisha wanatumia vyandarua hivyo kujikinga na malaria na siyo vinginevyo.