KAYA 56,363 zimehesabiwa hadi kufikia leo Agosti 25 ikiwa ni asilimia 37.07 ya Kaya 152,332 zinazotarajiwa kuhesabiwa katika zoezi la sensa ya watu na makazi lililoanza Agosti 23.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa zoezi hilo, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko amesema hadi sasa zoezi linaridhisha na anauhakika hadi kufika tarehe 29 Kaya zote zitakuwa zimehesabiwa.
Pamoja na hayo, RC Mrindoko amewasisitiza wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa makarani huku akiwaonya wote watakaobainika kupostosha ikiwemo kuwapiga na kusambaza picha za makarani zisizo na maadili.
“Tuache mzaha na zoezi la Sensa, tuache kurusha picha ambazo hatuzielewi zimetoka wapi,tuache kurusha maneno au taarifa mbalimbali au sauti zinazohusiana na kuwakejeli makarani wa Sensa,zoezi la Sensa ni la kisheria tusifanye mzaha huo”alisema