TAKRIBANI kaya 80,000 nchini Kenya zimeathiriwa na mvua kubwa, mafuriko na maporomoko ya ardhi wiki iliyopita, Naibu wa Rais amesema.
–
Huduma za dharura zinatumia helikopta kutoa msaada na uokoaji wa familia zilizoachwa, taarifa ya Rigathi Gachagua imeeleza.
–
Afrika Mashariki imekumbwa na mvua kubwa inayohusishwa na hali ya hewa ya El Niño, ambayo imeua makumi ya watu, ikiwa ni pamoja na 46 nchini Kenya.
–
Mafuriko pia yamesababisha vifo na nchini Somalia na Ethiopia.
–
Mvua hiyo imeelezwa na Umoja wa Mataifa kama tukio la kubwa katika karne.
Home Kaya 80,000 zapatiwa msaada Kenya
Comments are closed.