Kaze ajiunga Namungo

Aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Klabu ya Yanga Cedric kaze rasmi amejiunga na Klabu ya Namungo kutoka Lindi.

Taarifa iliyotolewa na klabu ya Namungo kupitia mitandao yake ya kijamii imeeleza kuwa kocha Kaze amesaini kandarasi ya miaka miwili ya kukinoa kikosi hicho.

Msimu uliopita kocha huyo raia wa Burundi alikuwa kwenye kikosi cha timu ya Yanga kilichotwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara na ubingwa wa kombe la shirikisho la Azam pamoja na kucheza fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Habari Zifananazo

Back to top button