Kaze: Wachezaji wana uchovu

KOCHA msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema uchovu wa wachezaji wao uliotokana na mechi za mashindano ya kimataifa unaweza kuwapa wakati mgumu kesho katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Azam Sports Federetion (ASFC), dhidi ya Geita FC.

Akizungumza na HabariLEO, kocha huyo ameeleza kuwa yeye na wenzake wa benchi la ufundi wamejitahidi kuiandaa timu yao vizuri ili kupata ushindi na kusonga mbele hatua inayofuata lakini anaamini haitokuwa rahisi kutokana na ubora waliokuwa nao Geita.

“Hatuwezi kuwadharau Geita sababu ni timu ambayo imekuwa na rekodi ya kutusumbua kila tunapokutana nayo, tumejipanga kupata ushindi kwa kutegemea uzoefu wa waliokuwa nao wachezaji wetu ingawa uchovu wa mechi za kimataifa bado unawasumbua,”amesema Kaze.

Kocha huyo amesema pamoja na changamoto hiyo lengo lao ni kuhakikisha wanafanya vizuri katika kila mechi ili kutetea taji hilo ambalo walilibeba msimu uliopita mbele ya Wagosi wa Kaya, Coastal Union uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x