Kaze:Moto utawaka

DAR ES SALAAM: Kocha wa Namungo Cedric Kaze amesema wachezaji wake hawapaswi kuogopa kucheza dhidi ya Yanga licha ya ubora walionao kwa sasa.

Kaze ameyasema hayo leo Septemba 19, 2023, wakati akizungumzia maandalizi ya mchezo wa kesho dhidi ya mabingwa hao watetezi wa ligi kuu Tanzania bara.

Kaze amesema tofauti na wengi wanavyofikiri kuwa utakuwa mchezo wa upande mmoja yeye amewaandaa vyema wachezaji wake na watakuja na utofauti mkubwa.

Advertisement

“Ninakwenda kucheza na timu ambayo nilikuwa nayo msimu uliopita, timu ambayo ipo kwenye kiwango bora kwa sasa, tunataka kwenda kuanza vizuri mchezo wa kesho” itakuwa ni siku muhimu sana kwangu ninakutana na timu ambayo niliifundisha kwa zaidi ya miaka miwili.

Katika hatua nyingine nyota wa Namungo Jacob Massawe, amesema hakuna timu isiyofungwa hivyo lolote linaweza kutokea, na wachezaji wa timu hiyo wanajivunia uwepo wa kocha Cedric Kaze ambaye amewapa mbinu za kucheza dhidi ya Yanga.

 

 

3 comments

Comments are closed.