Kazi: Tupo imara kuivaa Geita

BEKI wa klabu ya Simba, Hussen Kazi amesema kuwa kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Geita Gold Fc wamejiandaa vizuri kwani kila mchezaji anafahamu umuhimu wa mchezo huo na kuingeza  kuwa kama wachezaji wapo tayari kupambana ili kuwapa furaha mashabiki wao.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake kwenye mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo dhidi ya wachimba dhahabu wa Geita Gold Fc utakaochezwa kwenye dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza Februari.

12.2024 kazi ameongeza kuwa kama wachezaji wameshasahau matokeo ya mchezo wa mwisho uliopita dhidi ya Azam FC na sasa wameelekeza ngungu zao kwenye mchezo huo.

Hadi sasa kwenye msimamo wa Ligi Kuu Simba inashika nafasi ya 3 wakiwa na pointi 30 huku wakiwa wamecheza michezo 13.

Habari Zifananazo

Back to top button