Kerege maji bwerere mwishoni mwa mwaka

WAKAZI wa vitongoji vya Nyakahamba na Kitonga Kata ya Kerege Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, wamehakikishiwa huduma ya maji ifikapo Desemba mwaka huu kupitia mradi wa uboreshaji huduma ya maji kutoka Bagamoyo hadi Makongo.

Meneja wa Mkoa wa Kihuduma wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) Mapinga, Abraham Mwanyamaki alisema hayo mwishoni mwa wiki.

Alisema mradi huo utamaliza changamoto ya majisafi na akasema katika Kata ya Kerege huduma ya majisafi ni nzuri isipokuwa katika vitongoji hivyo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bagamoyo, Mohamedi Usinga aliwaomba Dawasa wasimamie mradi kwa karibu zaidi ili ukamilike haraka.

Diwani wa Kata ya Kerege, Ngatiruka Said Abdalah, aliwataka wananchi wa vitongoji hivyo viwili kuwa na subira na kuiamini serikali kwamba itawaondolea changamoto ya maji.

Mradi wa uboreshaji huduma ya maji kutoka Makongo hadi Bagamoyo, unalenga kuboresha upatikanaji wa huduma kwa wakazi tabribani 450,000.

Umehusisha ujenzi wa matangi matatu Vikawe, Mbweni na Tegeta A yenye ujazo wa lita milioni tano kila moja na yatahudumia wakazi wa maeneo ya Mapinga, Mabwepande, Bunju, Mbweni, Wazo, Tegeta A, Madale, Goba na Makongo.

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button