Kero 117 zaibuliwa Takukuru Kigoma

JUMLA ya kero 117 zimeibuliwa na wananchi kupitia vikao vya kata viliivyofanywa na Taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) mkoa Kigoma kupitia program yake ya mikutano ya kata maarufu kama Takukuru Rafiki.

Mkuu wa Dawati la Elimu kwa Umma Mkoa Kigoma ,Leonida Mushama amesema hayo wakati akitoa taarifa ya utekelezaji ya taasisi hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu Julai hadi Septemba mwaka huu kwa niaba ya Mkuu wa Takukuru Mkoa Kigoma, Stephen Mafipa.

Mushama amesema kuwa katika mikutano hiyo, Takukuru ilitembelea kata 15 za wilaya na mkoa Kigoma na kufanya vikao ambavyo vimefanikishwa kuibuliwa kero hizo.

Amesema kuwa katika kero zilizotolewa sehemu kubwa zilikuwa zikihusu idara ya afya, wananchi wakilalamikia upungufu wa watumishi na uhaba wa dawa, kwa sekta ya elimu ilihusu upungufu wa walimu,ubovu, upungufu wa madawati na miundombinu duni ya shule.

Masuala mengine ni migogoro ya ardhi, umeme, malalamiko ya watumishi kutolipwa fedha za uhamisho, ambapo hadi sasa kero 70 zimetatuliwa na 47 zipo kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Eviessity
Eviessity
21 days ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ http://Www.Careers12.com

Last edited 21 days ago by Eviessity
Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x