Kero 4 kati ya nane za muungano zapatiwa ufumbuzi

KATIKA kuenzi na kudumisha muungano, serikali kwa mwaka 2022/23, imejadili   hoja nane  za Muungano ambapo hoja nne  zilipatiwa ufumbuzi na kuondolewa katika orodhaya hoja za
Muungano.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba, akiwasilisha bajeti ya serikali jana amesema  hoja zilizopatiwa ufumbuzi ni malalamiko ya wafanyabiashara wa zanzibar
kutozwa kodi mara mbili; kodi ya mapato (Pay As You Earn -PAYE) na kodi ya zuio (Withholding Tax); mkataba wa mkopo wa fedha za mradi wa
ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume (Terminal III); na ongezeko la gharama za umeme kutoka Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO) kwenda Shirika la Umeme la Zanzibar (ZECO).
“Napenda kulihakikishia bunge, Serikali zote mbili zina nia ya dhati na thabiti katika kuhakikishakuwa, hoja za Muungano zilizopo na zitakazojitokeza
zinashughulikiwakwa wakati ili kuulinda na kuudumisha Muungano wetu adhimu.”Amesema
Amesema Serikali inatambua
kuwa Muungano  ni Tunu ya Taifa  na
ndio utambulisho wetu duniani, hivyo ni jukumu la kila mmoja kuulinda, kuudumisha na kuuenzi.
1 comments

Comments are closed.