“Kesho sio mechi tu, ni fainali”

DAR ES SALAAM: NAHODHA msaidizi wa Simba, Mohamed Hussein amesema wachezaji wa timu hiyo wanautambua umuhimu wa mchezo wa kesho wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca.

 

Akizungumzia maandalizi ya timu hiyo kuelekea mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam, nahodha huyo ametanabahisha kuwa mchezo huo umebeba ramani nzima ya timu yao kwenye michuano hiyo ya Vilabu Afrika.

“Wachezaji wa Simba tunajua wazi kuwa michezo iliyopita hatukuwa katika ule ubora wetu, tumeshasahau hayo, kesho tuna mchezo mpya kabisa, kwetu hii sio mechi bali ni fainali, tukishinda kesho tunarejesha ile imani ya kufuzu hatua inayofuata,” amesema mlinzi huyo.

 

Mpaka sasa Simba imecheza michezo mitatu wakiwa hawajashinda mchezo wowote, wakipata sare mbili na kupoteza mchezo mmoja huku wakiwa mkiani mwa Kundi B na alama zao mbili, huku Wydad ikiwa nafasi ya tatu na alama zake tatu nyuma ya Jwaneng Galaxy wenye alama nne na vinara Asec Mimosas wenye alama saba.

Habari Zifananazo

7 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button