Kesi 19 za ubakaji zawasilishwa mahakamani Shinyanga

JESHI la polisi mkoani Shinyanga limefanikiwa kufikisha kesi 19 mahakamani zaidi zinazotokana na tuhuma za makosa ya kulawiti na kubaka katika kipindi cha mwezi Oktoba mwaka huu.

Kamanda wa polisi mkoani hapa, Janeth Magomi amesema hayo jana mbele ya waandishi wa habari huku akieleza katika makosa hayo ipo kesi moja ya mtuhumiwa kudaiwa kutorosha mwanafunzi na tayari imetolewa hukumu ya kifungo cha miaka 30 kwenda jela.

Aidha Kamanda Magomi alisema ipo kesi moja ya shambulio la aibu ambapo mtuhumiwa alifikishwa mahakamani na kufungwa kifungo cha miaka 20 jela na faini ya Sh milioni 1.

“Kesi tatu za watuhumiwa wa makosa ya kubaka na kulawiti zilihukumiwa kifungo cha kati ya miaka 30 hadi kifungo cha maisha jela.”alisema Magomi.

Magomi alisema wamefanikiwa kukamata vifaa mbalimbali vya ramli chonganishi ikiwemo mifuko ya saruji 24,ndoo nne na makopo manne ya rangi yaliyoibiwa kwenye eneo la ujenzi wa nyumba za waathiri wa tope Mwadui wilayani Kishapu.

Kamanda Magomi alisema katika msako waliofanya kwa kipindi hicho waliweza kukamata gramu 2205 pamoja na kete 61 za dawa za kulevya aina ya bangi na pikipiki 11 zilizokuwa zikitumika kwenye uhalifu.

“Ninatoa wito kwa wananchi kufuata sheria za nchi na kutojihusisha na vitendo vya kiuhalifu na atakaye fanya hivyo atachukuliwa hatua za kisheria.”alisema Magomi

Habari Zifananazo

Back to top button