Kesi 42 kusikilizwa Mahakama ya Rufaa

NAIBU Msajili wa Mahakama ya Rufaa Tanzania, Charles Magessa amesema kuwa mahakama hiyo inatarajiwa kusikiliza kesi 42 katika kikao chake kilichoanza jana agosti 14 mwaka huu katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Magessa alisema kuwa katika kikao hicho ambacho kimeanza mkoani Arusha katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kitaongozwa na mwenyekiti jopo la majaji watatu jaji Mwanaisha Kwariko.

Alisema majaji wengine wataosikiliza kesi hizo ambazo ni kesi za jinai na mdai ni pamoja na jaji Barke Salehe,Jaji Zepharine Galba na Jaji Amour Hamisi.

Msajili huyo alisema kikao hicho kinatarajiwa kumalizika Septemba Mosi mwaka huu katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Alisema vikao vyote vinatarajiwa kuanza majira ya saa 2.30 asubuhi na kumalizika majira ya saa 9.30 mchana na kila kitu kiko sawa kwa ajili ya vikao hivyo.

Habari Zifananazo

Back to top button