Kesi ya wanaodaiwa kuvujisha mtihani yanguruma 

UPANDE wa mashitaka katika kesi ya kuvujisha mtihani wa taifa wa darasa la saba mwaka 2022, inayowakabili watu tisa umedai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakakamilika.

Wakili wa Serikali Yousuf Aboud ameeleza hay oleo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, wakati kesi hiyo ilipotajwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Pamela Mazengo anayeisikiliza kesi hiyo.

Aboud alidai bado wanaendelea na upelelezi wa kesi hiyo, hivyo aliiomba mahakama ipange tarehe nyingine ya kutajwa ambapo ilipangwa Februari mwaka huu.

Advertisement

Washitakiwa katika kesi hiyo ni Johnson Ondieka, Patrick Chawawa, Theresia Chitanda, Elinami Sarakikya, Joyce Nkomola , Lloyd Mpande, Olomy Odongo, Docras Muro na Alcherous Malinzi.

Katika kesi hiyo inadaiwa kuwa kati ya Oktoba 2 hadi 12 mwaka 2022, washitakiwa hao wakiwa Dar es Salaam,  walisambaza mtihani huo kupitia mtandao wa kijamii wa Whatsapp na Telegram na kusababisha kuvuja kwa watu ambao hawakuwa na mamlaka ya kuusimamia.

Inadaiwa kuwa katika tarehe hizo mshitakiwa Malinzi akiwa Dar es Salaam alitengeneza nyaraka za uongo kuonesha kama mtihani wa Taifa wa Darasa la saba wa somo la Uraia, na somo la Maadili na Maalifa ya Jamii akionesha ni halali iliyotolewa na Baraza la Taifa la Mitihani, wakati akijua si kweli.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *