Khalfan Khalmandro afariki dunia

MUONGOZAJI na mtayarishaji wa video za muziki nchini, Khalfani Khalmandro
DAR ES SALAAM: MUONGOZAJI na mtayarishaji wa video za muziki ‘vichupa’ nchini, Khalfani Khalmandro amefariki dunia alfajiri ya leo katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) jijini Dar es Salaam.
 
Khalmandro amekutwa na umauti baada ya siku kadhaa kulazwa hospitalini kwa tatizo la damu kuvilia kwenye ubongo lililomsababishia kupata Kiharusi ama kupooza upande mmoja wa mwili wake.
 
Enzi za uhai wake, Khalfan alijipatia umaarufu kwa kuongoza video za wanamuziki kadhaa, wakiwamo Aslay, Navy Kenzo, Christian Bella, Baby Madaha, Chin Bees, Shilole, Linah na wengine wengi.
 
Miongoni mwa vichupa vilivyowahi kupita katika mikono ya muongozaji huyo ni pamoja na video ya Aah Wapi ya Country Boy, Bishoo ya Quick Rocka ft Young Dee, I just Wanna love you ya Navy Kenzo, YESA Marioo Ft Chino Wanaman na nyingine nyingi.