Kiama cha wauzaji, watumiaji dawa za kulevya chaja

KAMISHINA Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya DCEA), Aretas James Lyimo ametangaza operesheni maalum nchi nzima ya Kupambana na Dawa za Kulevya
Akizungumza  na HabariLEO amesema mamlaka Mamlaka yake imeweka mipango dhabiti ya kuhakikisha wanakabiliana na changamoto hiyo
“Kwa hiyo nitoe wito kwa watumiaji wa dawa za kulevya kuacha wenyewe kutumia dawa za kulevya, lakini pia kwa wale wauzaji na wasambazaji wa dawa za kulevya kuacha kabisa hiyo biashara ya dawa za kulevya.
“Kuanzia sasa tunafanya operesheni kabambe nchi nzima, lakini tutahakikisha vijiwe vyote vya wauzaji, na watumiaji wa dawa za kulevya tunavisambaratisha.” Amesema